KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 20 Aprili 2014

MKUU WA WILAYA YA KALAMBO MH. MOSHI CHANG'A AFARIKI DUNIA

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang'a ( enzi za uhai wake ) akizungumza katika mahafali ya pili ya chuo cha ualimu St. Aggrey Chanji.

Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Mh Moshi Chang'a amefariki dunia leo jioni katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akitibiwa maradhi ya Kisukari.

LIGI KUU UINGEREZA, MANCHESTER UNITED YAKUBALI KIPIGO CHA MABAO 2-0 TOKA KWA EVERTON

 Mchezaji Leighton Baines akiifungia timu yake ya Everton bao la kwanza kwa mkwaju wa penati kunako dakika ya 28 ya mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Manchester United ambayo msimu huu imepoteza kabisa mwelekeo. 

Penati hiyo ilipatikana baada ya beki wa Man U, Phil Jones kuunawa mpira 
ndani ya 18 wakati akiwa katika harakati za kuondoa hatari langoni mwao. 

Katika mchezo huo, Everton walionekana kuelewana sana uwanjani mwanzo hadi mwisho wa mchezo huku wakishangiliwa sana na mashabiki wao.
 Mirallas akiifungia Everton bao la pili kunako dakika ya 43 huku mlinda mlango wa Mashetani wekundu David De Gea akijaribu kuucheza mpira huo bila ya mafanikio. 

Kwa matokeo hayo katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Goodison Park, Everton wamefikisha pointi 69 na kuendelea kubaki nafasi ya tano, huku Man U wakiendelea kubaki nafasi ya saba wakiwa na pointi 57
 Duh na leo tena tumepigwa, mwaka huu kila timu inajichukulia pointi kama tumelala!! Wayne Rooney akiwa mnyonge baada ya kupigwa 2-0 na Everton
HIVI NINAYO SHUHUDIA NI KWELI AU NIPO NDOTONI!!! Kocha wa Manchester United David Moyes akiwa haamini kipigo alichokipata

LIGI KUU UINGEREZA, PODOLSKI NA RAMSEY WAIBEBA ARSENAL IKIICHAPA HULL 3-0

 Mabao matatu yaliyopatikana katika kipindi cha kwanza nacha pili yameiwezesha Arsenal kufikisha pointi 70 na kusimama katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza. 

Ikicheza ugenini dhidi ya Hull City, Arsenal ilipambana na kupata mabao hayo kupitia kwa Aaron Ramsey dakika ya 31, huku Podolski akitumbukiza kambani mabao mawili, dakika za 45 na 53. 

Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki 24,762 Arsenal walionekana kulisakama lango la Hull City kwa muda mrefu wa mchezo
 Mchezaji Podolski akipongezwa na wachezaji wenzake, Olivier Giroud ( aliyemrukia ) na Aaron Ramsey baada ya kufunga goli
Podolski akijipinda na kuachia shuti kali lilikwenda kimiani na kuiandikia Arsenal bao la pili. 

Mchezo unaoendelea sasa ni kati ya Manchester United dhidi ya Everton ukiwa katika dakika ya 31, na tayari Everton wanaongoza kwa bao 1-0 lilipatikana kwa njia ya penati dakika ya 28 mfungaji akiwa ni Baines baada ya beki wa Man U Jones kuunawa mpira ndani ya 18 katika harakati za kuokoa mashambulizi langoni mwao. 

Everton wanawaendesha puta Man U. Tutawapa matokeo kamili baada ya mchezo huo kumalizika

WATU 6 WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE 5 WANA HALI MBAYA KUFUATIA AJALI ILIYOTOKEA NAIVASHA

Watu sita wameripotiwa kufariki na wengine watano wana hali mbaya na wamelazwa katika hospitali ya Kijabe, kufuatia ajali iliyohusisha basi la abiria ( matatuu ) na lori la mizigo eneo la Kinungi katika barabara kuu ya Naivasha - Nairobi. 

Mmoja wa majeruhi, Lucy Nyakanini ( pichani ) amesema dereva wa basi alilokuwa amepanda alikuwa anajaribu kulipita basi lingine lililokuwa mbele yao, ndipo walipogongana na lori lililokuwa linakuja mbele yao.

HATA LONDON PIKIPIKI ZA VESPA ZIMEJAA TELE KAMA ZILIVYOJAA ZANZIBAR

 Sio Zanzibar tu pikipiki hizi almaarufu kwa jina la Vespa zimejaa, bali hata kwa wenzetu bado ni usafiri unaotumiwa na kupendwa na wengi. Hapa Vespa hizi zikionekana zikikatiza mitaa ya jiji la London nchini Uingereza

LIGI KUU UINGEREZA, LIVERPOOL NJIA NYEUPE YA UBINGWA 2014

 Timu ya soka ya Liverpool imeendelea kujisafishia njia ya kuutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza msimu huu, baada ya leo kuifunga Norwich mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa nyumbani wa Norwich, Carrow Road na kushuhudiwa na mashabiki 26,857
 Katika mchezo huo, Liverpool walijipatia bao la kwanza kupitia kwa Sterling kunako dakika ya 4 ya kipindi cha kwanza na kufunga tena bao la tatu dakika ya 64. Luis Suarez aliifungia Liverpool bao la pili dakika ya 11 ya mchezo, na mabao ya Norwich yalifungwa na Hooper dakika ya 53 na Snodgrass dakika ya 77.
Kwa matokeo hayo Liverpool imefikisha pointi 80, tano zaidi ya Chelsea yenye pointi 75 ambayo jana ilikubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Sunderland. Manchester City wapo nafasi ya tatu na pointi 71. 

Hivi sasa Arsenal wanacheza na Hull City, na hadi dakika ya 16 tunaenda mitamboni timu hizo zilikuwa bado hazijafungana. 

Tutawaletea matokeo baada ya mcheo huo kumalizika

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR BALOZI SEIF AFUNGA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO


Wazanzibari na Watanzania wametanabahishwa kwamba baadhi ya mambo yaliyokuwa yakilalamikiwa kwa muda mrefu na Zanzibar yatokanayo na kero za Muungano yanaweza kushindikana kurekebishwa kisheria endapo mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya ya Muungano hautafikia lengo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitanabahisha hilo wakati akilifunga Kongamano la siku moja la Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort iliyopo Mazizini Nje kidogo ya Mjini Zanzibar.

Balozi Seif alilitolea mfano Suala la Mafuta na Gesi ambalo Zanzibar inataka litolewe kabisa katika mambo yaliyomo ndani ya Muungano linaweza lisifikie usuluhishi kwa vile ni suala linalohitaji marekebisho ya kina ya Kisheria.

PAPA AONGOZA MISA YA SIKUKUU YA PASAKA

 Maelfu ya waumini wa dini ya Kikristo waliokusanyika katika viwanja vya kanisa la St.Peters mjini Vatican wakifuatilia misa ya Pasaka iliyokuwa ikiendeshwa na Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis leo ameongoza maelfu ya waumini wa dini ya Kikristo katika misa ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka, misa iliyofanyika katika kanisa la St.Peters Vatican. 

Pasaka ni siku ambayo Wakristo wanaadhimisha kufufuka kwa Yesu Kristo. 

Katika misa hiyo, Papa Francis amesisitiza amani, na mazungumzo yenye kufikia muafaka huko Ukraine na Syria, na pia Papa Francis amesisitiza kufikia mwisho kwa mashambulizi yanayofanywa dhidi ya Wakristo nchini Nigeria
Katika misa hiyo, Papa pia katika mahubiri yake amewaombea watu masikini na waliosahaulika katika jamii. Amewataka watu wote duniani kuwa na upendo dhidi ya watu masikini kwa kuwaombea na pia kuwasaidia

WALIOPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA MAPOROMOKO YA THELUJI MLIMA EVEREST WAFIKIA 13

 Watu 13 ambao wanashughulika na shughuli za kuwasindikiza watalii kukwea milima nchini Nepal wamekufa baada ya kuporomokewa na theluji katika mlima Everest. Hadi kufikia jana jumamosi waongoza watalii wengine watatu walikuwa bado hawajaonekana
                                                             Maporomoko ya Theluji yalivyokuwa 

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR MAALIM SEIF AHIMIZA UPANDAJI WA MITI


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipanda mti katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti Kitaifa, katika eneo la barabara ya Jendele/Unguja Ukuu


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipanda mti katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti Kitaifa, katika eneo la barabara ya Jendele/Unguja Ukuu


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti Kitaifa, katika eneo la barabara ya Jendele/Unguja Ukuu


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti Kitaifa, katika eneo la barabara ya Jendele/Unguja Ukuu


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili, Affan Othman Maalim (kushoto) katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti Kitaifa, barabara ya Jendele/Unguja Ukuu


Baadhi ya wananchi wakishuhudia uzinduzi wa zoezi la upandaji miti Kitaifa, katika eneo la barabara ya Jendele/Unguja Ukuu ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Na: Hassan Hamad (OMKR). 

Jamii imehimizwa kukitumia kipindi hiki cha mvua za masika kupanda miti kwa wingi, ili kurejesha hadhi ya Zanzibar ya kuwa “Visiwa vya Kijani”.
Wito huo umetolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, wakati akizindua zoezi la upandaji miti Kitaifa katika barabara ya Jendele Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema kwa kiasi kikubwa jamii imepoteza utamaduni wa asili wa kupanda na kutunza miti, hali inayopelekea kutoweka kwa baadhi ya miti mikubwa ya matunda na viongo katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.

Hivyo ameziagiza serikali za Mikoa na Wilaya kusimamia utunzaji wa miti inayopandwa, ili kuhakikisha kwamba inakuwa vizuri na kuleta ustawi uliokusudiwa katika utunzaji wa mazingira na kuongeza kipato cha wananchi na Taifa kwa ujumla.

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AZUNGUMZIA SABABU ZA ONGEZEKO LA MARADHI YA KISUKARI NA SHINIKIZO LA DAMU


Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanafunzi wa Udaktari Tanzania { TAMSA } kwa kushirikiana na wizara ya afya Zanzibar wakiendesha zoezi la siku nne la kupima, kutoa elimu na huduma za Dawa kwa wagonjwa wa maradhi ya Kisukari na Shinikizo la Damu hapa Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipima damu mara baada ya kufungua kampeni ya kutoa huduma za shinikizo la Damu na Kisukari katika majengo ya Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni MnaziMmoja Mjini Zanzibar.
Mradi huo unasimamiwa na Jumuiya ya Chama cha Wanafunzi wa Udaktari Tanzania { TAMSA } kwa kushirikiana na Chuo mcha Kimataifa cha Udaktari Tanzania { imtu } 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Kimataifa cha Udaktari Tanzania { IMTU } Profesa Flora Fabian Mbatia kwenye majengo ya Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.

                                             Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ .

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba ukosefu wa mlo kamili uliokusanya matunda na mboga za kutosha, uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kiholela, tabia ya uvivu na ongezeko la uzito ndio sababu kuu zinapelekea ongezeko kubwa la maradhi ya Kisukari na shindikizo la Damu miongoni mwa wanaadamu.

Alisema utumiaji wa vyakula hivyo kwa mpango maalum pamoja na ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya ndio njia pekee inayoweza kuzuia kuripuka kwa maradhi hayo kwa zaidi ya asilimia 80%.

Balozi Seif alisema hayo katika sherehe ya ufunguzi wa Kampeni ya kutoa huduma za Shindikizo la Damu na Kisukari zilizoandaliwa na Jumuiya ya Chuo cha Udaktari Tanzania na kufanyika ndani ya Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Kampasi ya Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni Vuga Mjini Zanzibar.

UKITOKA HAKIKISHA UNAVAA GAUNI LITAKALOKUFANYA UPENDEZE ZAIDI

 


VIFO VYAONGEZEKA KIVUKO CHA KOREA KUSINI

 Ndugu na jamaa wa waliozama na kivuko huko Korea Kusini wameshikwa na hasira na kulalamikia zoezi la uokoji, wakisema hawaridhishwi na kasi ya uokoaji wa ndugu zao katika kivuko hicho kilichozama jumatano
 Polisi waliongezwa kuimarisha ulinzi ili kukabiliana na ndugu hao wenye hasira.Polisi walifanikiwa kuwazuia zaidi ya watu 100 waliotaka kuingia Seoul kutoka kisiwa cha Jindo
 Baada ya juhudi za siku tatu, hatimaye wapiga mbizi jana walifanikiwa kuingia ndani ya kivuko hicho na kutoa miili 22 na kufanya idadi ya waliofariki dunia kutokana na kuzama kwa kivuko hicho kufikia 54. 

Mpaka sasa watu 174 ndio waliookolewa na wengine 248 bado hawajaonekana
Waokoaji wakibeba moja ya miili ya waliopoteza maisha baada ya kuzama kwa kivuko hicho

LIGI KUU UINGEREZA, CHELSEA YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA SUNDERLAND

 Timu ya soka ya Sunderland jana iliitibulia Chelsea kukamata usukani wa ligi kuu Uingereza baada ya kuifunga mabao 2-1 katika mchezo ambao mwamuzi Mike Dean alionekana kushindwa kuumudu vyema
 Katika mchezo huo, Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Samule Eto'o kunako dakika ya 12, hata hivyo Sunderland ambao niwa mwisho katika msimamo wa ligi pamoja na ushindi wa jana, walisawazisha bao hilo kupitia kwa muuaji wao Wickham kunako dakika ya 18 nala pili kupitia kwa Borin dakika 82 kwa penati. 

Kwa matokeo hayo bado Chelsea wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 75 nyuma ya Liverpool wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 77
Kocha msaidizi wa Chelsea Rui Faria akimlalamikia mwamuzi Mike Dean baada ya kutoa penati kwa Sunderland

MIYEYUSHO NA CHEKA WASHINDWA KUNG'AA PTA, MIYEYUSHO APIGWA

Bondia Fransic Cheka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde naGavad Zohrehvand wa Iran wakati wa mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam mpambano huo uliamliwa kwa droo ya kufungana point
Bondia Francis Cheka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Gavad Zohrehvand wa Iran wakati wa mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam mpambano huo uliamliwa kwa droo ya kufungana point
Bondia Sukkasem Kietyongyuth kutoka Thailand kulia akiwa amemkalisha bondia Francis Miyeyusho katika raundi ya kwanza ya mpambano wa raundi kumi na kushinda kwa K.O.
Bondia Fransic Miyeyusho kushoto akijitutumua kupigana na Bondia Sukkasem Kietyongyuth kutoka Thailand. Miyeyusho alipigwa raundi ya kwanza bila huruma