.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 23 Aprili 2014

BALAA CHELSEA!! TERRY NA CECH MAJERUHI, KUIKOSA ATLETICO MADRID WIKI IJAYO

 Mlinda mlango tegemezi wa matajiri wa London Chelsea, Petr Cech ameumia mkono wake wa kulia katika mchezo wa nusu fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya usiku wa kuamkia leo wakati akiondoa hatari langoni kwake. 

Mlinda mlango huyo mahiri mwenye miaka 31, aligongana mshambuliaji wa Atletico Madrid Raul Garcia langoni mwa Chelsea katika mchezo huo uliomaliza kwa timu hizo kutofungana.
 Cech akiangukia mkono wake wa kulia pamoja na mshambuliaji wa Atletico Madrid Raul Garcia 
                                      Cech akiondolea uwanjani baada ya kuumia mkono wake.
Naye nahodha wa Chelsea John Terry aliondolewa uwanjani baada ya kuumia kifundo cha mguu wake katika mchezo huo. 

Kwa maana hiyo, Cech na Terry wataukosa mchezo wa marudiano wa nusu fainali ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid utakaochezwa wiki ijayo mjini London.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni