.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 23 Aprili 2014

KIJANA ALIYESAFIRI KWA KUTUMIA TAIRI LA NDEGE HUKO MAREKANI, AMESEMA ALITAKA KWENDA SOMALIA KWA MAMA YAKE

 Kijana mwenye umri wa miaka 15 aliyefanikiwa kusafiri kwa kijificha katika tairi la ndege kutoka San Jose, California hadi Maui, Hawaii bila kupata matatizo yeyote, amesema kuwa alikuwa anataka kusafiri hadi Afrika, Somalia kumtafuta mama yake ambaye hajamuona toka akiwa na umri wa miaka miwili. 

Kijana huyo ambaye majirani wamemuelezea kuwa ni kijana mpole na mtaratibu sana mtaani kwao huko Santa Clara Califorinia, alidandia tairi la ndege ya Hawaiian Arline bila kuonekana na kusafiri angani kwa saa tano huku akikatiza bahari ya Pacific. 

Meneja wa uwanja wa ndege wa Hawaii, Marvin Moriz amesema kijana huyo ambaye hakutajwa jina lake kuwa, amewaambia maafisa wa uwanjani hapo kuwa hataki kurejea nyumbani kwao.
Alikamatwa baada ya kuonekana akikatiza uwanjani katika njia ya kutua na kurukia ndege, na baadaye alipelekwa hospitali. 

Kabla ya kudandia katika tairi hilo la ndege, kijana huyo alitumia zaidi ya masaa sita akiangalia mazingira ya uwanja wa San Jose akiwa nje ya uzio wa uwanja huo. 

Hata baada ya kutoonekana nyumbani kwao kwa zaidi ya saa 36, familia yake haikutoa taarifa polisi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni