.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 23 Aprili 2014

MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI JOE BIDEN AITAKA URUSI KUMALIZA HARAKA MGOGORO WA UKRAINE

 Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden ( pichani ) ameitaka Urusi kupunguza maneno na badala yake sasa ifanye kazi kwa vitendo kuhakikisha inamaliza mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Ukraine. Makamu huyo wa Rais wa Marekani aliyasema hayo jana jumanne alipokuwa katika ziara nchini humo.
 Biden ( kushoto ) aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari huku akiwa ameongozana na Waziri Mkuu wa Ukraine, Arseniy Yatsenyuk ( kulia ), na kusisitiza kuwa Marekani ipo tayari kulisaidia taifa hilo kujijenga upya kufuatia mgogoro huo uliosababisha ghasia na kufanya uharibifu mkubwa wa majengo ya serikali. 

Makamu huyo wa Rais wa Marekani ambaye pia alizungumza na wabunge wa Ukraine, ameitaka Urusi kuhakikisha inaacha kuchochea maandamano nchini Ukraine na kuliachia jimbo la Cremia ambalo lilijitangazia kujiengua Ukraine na kujiunga na Urusi.
Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden ( kulia ) akisalimia na mmoja wa wabunge wa Ukraine mara baada ya kuzungumza na wabunge hao mjini Kiev. 

Makamu huyo wa Rais ameanza safari ya kurejea Washington DC akitokea Ukraine

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni