.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 23 Aprili 2014

NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA, USIKU WA LEO NI REAL MADRID DHIDI YA BAYERN MUNICH

 Wachezaji wa timu ya soka ya Bayern Munich wakijifua katika uwanja wa Rayo Vallecano mapema leo asubuhi kabla ya usiku wa leo kucheza na Real Madrid katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali, ligi ya mabingwa barani Ulaya. 

Mchezo huo unatazamiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na umahiri wa vikosi vyote viwili vilivyojaa wachezaji wenye viwango vikubwa. 
Mchezo wa leo utachezwa katika uwanja wa nyumbani wa Real Madrid wa Santiago Bernabeu, huku nyota wa kikosi hicho Cristiano Roanldo akitarajiwa kushuka uwanjani kuwakabili Bayern Munich. 
Mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d'Or alikosa michezo minne ya timu yake, ukiwemo ule walioshinda mabao 2-1 dhidi ya Barcelona kwenye fainali ya kombe la Copa Del Rey kutokana na kusumbuliwa na goti.
PACHA WA REAL MADRID!! Cristiano Ronaldo na Gareth Bale wakijifua tayari kwa mchezo wa leo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni