Watu waliofariki dunia baada ya kuzama kwa kivuko huko Korea Kusini jumatano iliyopita sasa wamefikia 150 huku wengine 152 wengi wao wakiwa wanafunzi wa shule iliyopo Ansan nje ya jiji la Seoul wakiwa bado hawajaonekana mpaka sasa.
Pamoja na juhudi kubwa zilizofanywa na wazamiaji toka kutokea kwa ajali hiyo ya kivuko kilichokuwa kinaelekea katika kisiwa cha kusini cha Jeju, lakini bado kumekuwa na lawama kutoka kwa ndugu waliopoteza maisha wakisema zoezi la uokoji linafanyika kwa kasi ndogo.
Kati ya wahusika 29 wa kivuko hicho, ni 22 tu waliosalimika huku 11 wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka kufuatia ajali hiyo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni