.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 31 Julai 2014

DK KAMAN AHIMIZA WAWEKEZAJI KWENYE SAYANSI NA TEKNOLOJIA WAENDE BUSEGA

Waziri wa maendeleo ua mifugo na uvuvi nchini Dk Titus Mlengeya Kamani.

                                               Na:Shushu Joel wa Rweyunga Blog, Simiyu

Waziri wa maendeleo ua mifugo na uvuvi nchini Dk Titus Mlengeya Kamani amesema kuwa nchi za Afrika haziwezi kuendelea pasipo kuwekeza katika Sayansi na Teknlojia vijijini hasa kando kando ya ziwa Victoria.

Ametaka wawekezaji hao kuweza kuja Busega, na pia uwekezaji huo uzingatie maabara ya kisasa kwa shule za sekondari na vyuo ili kuweza kutoa msukumo kwa vijana wa Busega na Watanzania kwa ujumla ili kuweza kupata maendeleo ya kutosha na yenye tija kwa taifa.

Dk Kaman ametoa rai hiyo alipokuwa akizindua jengo la maabara katika shule ya sekondari ya Badugu na kisha kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo iliyoko wilayani Busega mkoani Simiyu.

Aliongeza kuwa Aayansi na Teknolojia vipewe kipaumbele ili kila nchi hapa duniani iwe na wataalamu wa kutosha na ziondokane na utegemezi wa wataalamu toka nchi jirani.

Aliongeza kuwa sasa ni wakati wa kuhakikisha elimu inapanda kwa kiwango kikubwa na kwa kasi, ikiwemo ajira kwa vijana ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.


Pia ni vyema sasa tukawapeleka watoto wetu wakike shule ili nao waweze kuwa kama wanawake wengine kwani mwanamke akiwezeshwa anaweza hivyo aliwasii wazazi kutowaozesha mabinti zao kwani hayo yamepitwa na wakati na sasa ni wakati wa wanawake , akiwatolea mfano wanawake wengi wanao wawakilisha wanawake wenzao katika nafasi mbalimbali za uongozi hapa nchi kama Spika wa bunge Anna makinda, Asha Rose Migiro, Sophia samba na wengine wengi duniani.

Hivyo Dk Kaman aliwataka wawekezaji waweze kuwekeza maeneo ya busega ili waweze kutoa elimu pia ya unyanyasaji kwa wanawake kwani bado kuna watu vijijini wanaamini motto wa kike apaswi kusoma yeye ni kuolewa tu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni