Serikali ya Liberia imetangaza
kufunga shule zote nchini humo katika jitihada za kuzuia kusambaa kwa
ugonjwa hatari wa Ebola.
Rais Ellen Johnson Sirleaf amesema
mbali na uamuzi huo baadhi ya jamii zitalazimika kutotoka katika
maeneo wanayoishi.
Vile vile watumishi wasio muhimu wa
serikali watatakiwa kutokwenda kazini na kubaki majumbani kwao, huku
jeshi la nchi hiyo likisambazwa kuhakikisha maagizo hayo ya serikali
yanatekelezwa.
Idadi ya watu waliokufa kwa kuugua
Ebola Afrika Magharibi sasa imefikia watu 672, kwa mujibu wa takwimu
mpya zilizotolewa na Umoja wa Mataifa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni