.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 24 Julai 2014

LOUIS VAN GAAL AANZA KWA KISHINDO MANCHESTER UNITED, AICHAPA LA GALAXY 7-0

Kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal amepata ushindi wa kwanza wa kishindo tangu achukue mikoba ya kuinoa timu hiyo baada ya kuifunga LA Galaxy kwa mbao 7-0 katika mchezo uliohudhuriwa na watazamaji 86,432 huko Rose Bowl, California.

Katika mchezo huo ambao kiungo wao mpya Ander Herrera alionyesha kiwango cha juu na kutoa mapande murwa yaliyochangia ushindi huo ambapo winga Ashley Young, beki Reece James, walifunga magoli mawili baada ya mshambuliaji Danny Welbeck kufunga goli la kuongoza katika dakika 13 za mwanzo. Rooney nae alipachika bao katika mchezo huo.
                                                                      Ander Herrera akiwajibika
                                                                       Shinji Kagawa akipiga shuti

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni