Ajali hiyo imetokea jana baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV linalofanya safari zake Mbeya - Tabora kugongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kwenda Mpanda.
Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, ACP Suzan Kaganda amesema kuwa ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani Sikonge.
Kamanda Kaganda amethibitisha idadi ya watu hao waliofariki pamoja na majeruhi baada ya kutembelea eneo la ajali na kufika katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni