.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 20 Agosti 2014

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO ( CHADEMA ) CHAKANUSHA KUHUSIKA NA MAUAJI YA MWANGOSI


Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika, akizungumza na waandishi wa habari.


Baadhi ya viongozi wa Chadema kutoka kushoto ni Ofisa Habari, Tumaini Makene, Mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika, Ofisa Mwandamizi Mafunzo na Uendeshaji, Mohamed Mtoi, na mwenye gwanda ni Katibu Mtendaji, Ofisi ya Katibu Mkuu, Victor Kimesera.Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya Chadema.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekana shutuma zilizoelekezewa kwao kuwa wanahusika na kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi.
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, Mhe. John Mnyika, ameeleza kuwa hawahusiki na mauaji hayo bali ni propaganda zinazoenezwa ili kuwasahaulisha wananchi juu ya suala la katiba linaloendelea.

Mnyika alieleza kuwa wanaoeneza habari hizo ni wale ambao wanataka kuizuia Chadema na Ukawa kwa ujumla kuendelea na harakati za kupigania katiba ya wananchi ikiwemo kufanyika maandamano ya kitaifa iwapo Rais Kikwete hataingilia kati kulisimamisha zoezi la katiba mpya.

                                                                                 (Picha na Gabriel Ng’osha/GPL)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni