Kutoka kulia ni Mhe. Balozi Dr.
Batilda S. Burian akifanya mazungumzo ofisini kwake na Mkurugenzi
Mkuu Mpya wa taasisi ya Shelter Afrique Bw. James Mugerwa(Katikati)
ambaye aliambatana na afisa wake Bw. Vipya Harawa (Kushoto) ambaye ni
Mkurugenzi wa masuala ya ushirikiano katika taasisi hiyo.
**************************
Bw. James Mugerwa, Mkurugenzi Mkuu
Mpya wa Taasisi ya Shelter Afrique yenye makao yake makuu hapa
jijini Nairobi amemtembelea Mhe. Balozi Batilda ofisini kwake kwa
ajili ya kujitambulisha kutokana na kuchaguliwa kwake hivi karibuni
kuwa Mkurugenzi Mpya wa Taasisi hii muhimu ambayo imekuwa
ikijishughulisha na utoaji wa mikopo nafuu kwa nchi wanachama wake
kwa ajili uendelezaji wa miji na makazi bora nafuu, ambapo Tanzania
ni moja ya nchi mwanachama katika taasisi hii.
Mhe. Batilda ni Balozi wa Tanzania
nchini Kenya ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye
Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UN-Habitat na UNEP yenye makao yake
makuu hapa Nairobi.
Katika mazungumzo, Bw. Mugerwa
alitoa shukrani za pekee kwa Tanzania kwa jinsi ambavyo imekuwa
ikitoa ushirikiano mkubwa kwa Taasisi hii na kuahidi kudumisha na
kuendeleza ushirikiano ambao umekuwepo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni