Nchi ya Liberia imepiga marufuku
watu kutembea usiku na kuzuia watu kutoka katika eneo moja la Jiji la
Monrovia katika jitihada za kukabiliana na mlipuko wa Ebola.
Rais Ellen Johnson Sirleaf amesema
amri hiyo ya kutotembea usiku inaanzia saa tatu usiku hadi saa kumi
na mbili alfajiri.
Amesema kuwa kila nyendo za watu
katika muda huo zitazuiliwa ambapo pia watu wa eneo la Magharibi mwa
Mji wa Monrovia hawaturuhusiwa kutoka nje ya eneo hilo.
Wakati huo huo madaktari watatu
wanaougua Ebola walioanza kutibiwa kwa kutumia dawa zilizo kwenye
majaribio wameonyesha dalili za kupata ahueni, Waziri wa Habari wa
Lewis Brown amesema.
Popo huyu mla matunda ndio anayesadikika kusambaza virusi vya Ebola
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni