.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 18 Septemba 2014

LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA, CHELSEA YABANWA NA SCHALKE

 Matajiri wa London Chelsea wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Stamford Bridge dhidi ya Schalke katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya jana usiku wameshindwa kuonyesha makali yao kama wafanyavyo katika mechi za ligi kuu Uingereza, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1.
Wageni Schalke walitangulia kufungwa kipindi cha kwanza, lakini walipambana kiume ugenini na kufanikiwa kutikisa nyavu za Chelsea kwa bao lililofungwa na nahodha wao Klaas-Jan Huntelaar katika kipindi cha pili cha mchezo na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Cesc Fabregas ( kushoto ) akiifungia Chelsea bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo dhidi ya Schalke katika mchezo wa ligi ya mbaingwa usiku wa kuamkia leo.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni