.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 18 Septemba 2014

LIGI YA MABINGWA ULAYA, BAYERN MUNICH YAICHAPA MANCHESTER CITY 1-0

 Manchester City bado wameonyesha wana safari ndefu ya kuja kufanya vyema katika michuano mikubwa nje ya ligi kuu ya Uingereza, baada ya usiku wa kuamkia leo kupokea kipigo cha bao 1-0 toka kwa wenyeji wao Bayern Munich katika mchezo wa ligi ya mabingwa Barani Ulaya, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Allianz Arena.

Wenyeji walijipatia bao lao katika dakika ya 89 mfungaji akiwa ni mchezaji Jerome Boateng ambaye hakufanya ajizi baada ya kupokea pasi ya Mario Gotze nae akautumbukiza mpira katika nyavu na kuwafanya wenyeji kuzoa pointi zote tatu.
Kizaa zaa langoni!! Mlinda mlango wa Manchester City, Joe Hart akijaribu kumzuia mshambuliaji matata wa Bayern Munich, Robert Lewandowski ambaye anaonekana kutaka kumpita mlinda mklango huyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni