.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 17 Septemba 2014

RAIS JACOB ZUMA AMESEMA RAIA 67 WA AFRIKA KUSINI WAMEKUFA KATIKA AJALI YA JENGO LA TB JOSHUA

Rais Jacob Zuma amesema raia 67 wa Afrika Kusini wamekufa katika tukio la kuanguka kwa jengo la kulala wageni la Muhubiri wa Nigeria, TB Joshua huko Lagos wiki iliyopita.

Rais Zuma amesema tukio hilo ni janga kubwa kuwahi kuwakuta raia wa Afrika Kusini wakiwa nje ya nchi katika historia ya nchi hiyo.

Vikosi vya uokoaji vya Nigeria vimesema karibu miili 70 ya watu imetolewa kwenye vifusi vya jengo hilo la ghorofa mbili.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni