.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 17 Septemba 2014

WANAKIJIJI NCHINI INDIA WANYOA VIPARA NA NDEVU KUOMBOLEZA KIFO CHA NYANI

Wanakijiji wapatao 200 nchini India wamenyoa vipara katika kuomboleza kifo cha nyani wa hekalu lao.

Nyani huyo wa hekalu alianguka kwenye bwawa na kufa maji baada ya kufukuzwa na mbwa.

Kwa kuhofia kifo cha nyani huyo kitasababisha bahati mbaya kwao, wanakijiji waliandaa mazishi ya nyani huyo kwa kumchoma moto kwa taratibu za mazishi ya Kihindu.

Pia wanavijiji wengine 700 wao nao walinyoa ndevu zao, katika kuomboleza kifo cha nyani huyo ambapo kwa kawaida mnyama huyo huchukuliwa kama Mungu kwa waumini wa thehebu la Kihindu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni