.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 23 Oktoba 2014

BONDIA THOMAS MASHALI AJIFUA KUMKABILI MKENYA HENRY WANDERA NOVEMBA MOSI FRIENDS CORNE



BONDIA Thomasi Mashali  yupo katika maandalizi mazito ya kumkabili bondia kutoka kenya Henry Wandera Novemba mosi katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam
Akizungumza wakati wa mazoezi yake juzi Mashali amesema kuwa yupo fiti wakati wowote yeye kufanya kazi hivyo haofii hata kidogo mpambano huo na kuwataka mashabiki wake waje waone anavyo mgalagaza vibaya sana siku hiyo mkenya Wandera

Mbali na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yatakayo wakutanisha Mbayo Ilunga na Fred Sayuni wakati Joseph Mbowe ataoneshana umwamba na Saidy Salum na Ramadhani Johncena ataoneshana ubabe na Baina Mazola

Mapambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita
katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo  kingilio ni shilingi, 7000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo 

Pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni