Waziri Mkuu wa Canada Stephen Harper
amesema nchi yake kamwe haitatishwa baada ya kutokea shambulio kubwa
katika bunge lake la taifa katika Jiji la Ottawa.
Bw. Harper amesema tukio hilo
linasisitiza Canada kuongeza maradufu jitihada zake za kupambana na
makundi ya ugaidi.
Mapema mtu mwenye silaha alimuua
mwanajeshi katika eneo la kumbukumbu ya vita la Ottawa, kabla ya
kuuwawa katika mapambano ya risasi na polisi ndani ya bunge.
Tukio hilo limetokea saa chache
baada ya Canada kuongeza kiwango cha hatari ya tishio la ugaidi.
Siku ya jumatatu mwanajeshi mmoja
aliuwawa kwa kugongwa na gari na kisha dereva wake kukimbia huko
Quebec, ambapo muhsika ni muislam aliyeslimu.
Picha ya mtuhumiwa aliyeuwawa baada ya kumuua mwanajeshi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni