Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe
(kushoto) akimkabidhi kadi ya CCM, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya
Nachingwea na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) wilayani humo, Manufreda Mathias Malenga. Kiongozi huyo
pamoja na wanachama wengine 22 wa chama hicho wamekikimbia chao chao na
kujiunga na CCM na kufanyiwa sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua
ambayo Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa
kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani
wilayani humo.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akimpongeza
Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema Kata ya Mtua, Habibu Oswadi (kushoto) baada ya
kukabidhi kadi ya chama chake. Kiongozi huyo wa Kata pamoja na wanachama wengine
22 wa chama hicho wamekikimbia chao chao na kujiunga na CCM na kufanyiwa
sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri Chikawe alikuwa
mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili
kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa
Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
hiyo, Abdalla Chikawe (wapili kulia kwa mgeni rasmi)
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza
na Viongozi wa CCM Wilaya, Kata pamoja na wananchi waliofurika katika Uwanja uliopo
jirani na Ofisi za CCM Kata ya Mtua katika sherehe kubwa ya kuwapokea viongozi wawili
na wanachama 21 wa Chadema waliojiunga na CCM wilayani humo. Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi ambapo
aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza
mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
Nachingwea, Regina Chonjo.
Mwanachama mpya wa CCM
ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Nachingwea na Kaimu
Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) wilayani Nachingwea, Manufreda Mathias Malenga akizungumza kwa hisia
baada ya kupewa nafasi kueleza furaha yake baada ya kukabidhi kadi ya Chadema
na kupewa kadi pamoja na sare za CCM. Malenga aliwashukuru Viongozi na wanachama
wa CCM kwa kumkaribisha katika chama hicho na kuahidi kutoa ushirikiano wake
ndani ya chama hicho. Kiongozi huyo pamoja na wanachama wengine 22 wa chama
hicho wamekikimbia chao chao na kujiunga na CCM na kufanyiwa sherehe kubwa
iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (katikati meza
kuu) alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare
za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe
(watano kulia waliosimama) akiwa na wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
baada ya kukikimbia chao cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Wananchama hao
23 wakiongozwa na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Nachingwea na
Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa chama hicho wilayani Nachingwea,
Manufreda Malenga (watano kushoto waliosimama) walifanyiwa sherehe kubwa
iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi aliwapokea
wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya
kupambana na upinzani wilayani humo. Picha
zote na Felix Mwagara.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni