.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 23 Oktoba 2014

DAKIKA MBILI ZA LALA SALAMA ZAWANUSURU ARSENAL NA KIPIGO DHIDI YA ANDERLECHT KATIKA LIGI YA MABINGWA ULAYA

 Ikicheza ugenini, washika bunduki wa jiji la London Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao Anderlecht katika mchezo wa ligi ya mabingwa Barani Ulaya, mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo.
Wakionekana kuukamia mchezo huo ili kuibuka na ushindi, vijana hao wanaonolewa na Mfaransa Arsene Wenger iliwabidi wafanye kazi ya ziada kuepuka aibu ugenini baada ya kujipatia mabao yao dakika za majeruhi. 

Mabao mawili ya dakika za lala salama yaliwekwa kimiani na Kieran Gibbs katika dakika ya 89 na dakika ya 90 Lukas Podolski akafunga bao la pili.
Wenyeji Anderlecht ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililowekwa kimiani na Andy Najar katika dakika ya 70 ya mchezo huo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni