Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja
akisaini katika Kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Afisa Mnadhimu
Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza,
Stephen Nzawila ambaye amefariki Jumapili tarehe 19 Oktoba, 2014 katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Mchungaji wa Kanisa la Moravian lililopo Ukonga, Banana
Relini Hansi Mwakijoja akiwaongoza Waombolezaji kwa sala kabla ya kuuaga rasmi
mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza ambaye
amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es
Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja
akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la
Magereza ambaye amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Dar es Salaam.
Baadhi ya Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa
wamejipanga katika mstari tayari kuuaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu
Msaidizi wa Jeshi la Magereza leo Oktoba 20, 2014 Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Mwili wa Marehemu unatajiwa kusafirishwa kesho kuelekea Tutuo Wilayani Sikonge,
Mkoani Tabora kwa Mazishi.
Mke wa Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la
Magereza akiwa na majonzi makubwa na waombolezaji kabla ya kuuaga rasmi mwili
wa mume wake ambaye amefariki Jumapili
Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Sehemu ya Waombolezaji waliojitokeza kuuaga mwili wa
aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza kwa
makini wasifu wa Marehemu kabla ya kuuaga rasmi leo Oktoba 20, 2014 Ukonga, Dar
es Salaam.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni