Mahakama ya Kislam imetekeleza
hukumu ya kupigwa mawe hadi kufa kwa kijana mmoja kusini mwa Somalia,
baada ya kumtia hatiani kwa kubaka mwanamke, taarifa za tovuti ya
Kiislam imeeleza.
Jaji aliagiza kijana Hasan Ahmad Ali
mwenye umri wa miaka 18, kumlipa fidia mwanamke huyo huyo ndama
mmoja, na kisha baadae kijana huyo kuuwawa.
Katika kesi hiyo kijana Ali
alikanusha kumbaka mwanamke huyo Fadumo Hasan Mohmoud mwenye umri wa
miaka 28.
Mwezi uliopita mwanamke mmoja
alipigwa mawe hadi kufa katika bandari ya Barawe, baada ya mahakama
ya Kiislam kumtia hatiani kwa kuolewa na wanaume wanne kwa wakati
mmoja.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni