.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 21 Oktoba 2014

LIGI KUU UINGEREZA, MANCHESTER UNITED YALAZIMISHA SARE YA 2-2 DHIDI YA WEST BROMWICH ALBION

 Manchester United bado inaendelea kupita katika wakati mgumu wa ligi kuu nchini Uingereza, baada ya jana usiku kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji wao West Bromwich Albion. 

Katika mchezo huo, West Brom ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 8 ya mchezo likifungwa na Stephane Sessegnon. 

Bao la pili la wenyeji hao liliwekwa kimiani na Saido Berahino katika dakika ya 66 ya kipindi cha pili cha mchezo.

Mabao ya Manchester United yaliwekwa kimiani na Marouane Fellaini aliyefunga bao katika dakika ya 48 na bao la pili likifungwa na Daley Blind kunako dakika ya 87 na kufanya matokeo ya mchezo huo wa ligi kuu nchini Uingereza kumalizika kwa timu hizo kufungana mabao 2-2.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni