.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 1 Oktoba 2014

LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA., PSG YAICHAPA FC BARCELONA 3-2 HUKU RAIS WA ZAMANI WA UFARANSA NA MWANAMUZIKI JAY NA MKEWE BEYONCE WAKISHUHUDIA KIPIGO HICHO

Ligi ya mabingwa barani Ulaya imeendelea usiku wa kumakia leo kwa kushuhudia wenyeji Paris St Germain ya Ufaransa wakiutumia vyema uwanja wao wa nyumbani kwa kuwachapa FC Barcelona waliosafiri kutoka nchini Hispania kwa jumla ya mabao 3-2. 

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Parc des Princes mjini Paris ulikuwa na ufundi wa hali ya juu toka kwa kila timu. 

Mabao ya PSG yaliwekwa kimiani na wachezaji David Luiz, Marco Verratti na Blaise Matuidi.
Mabao hayo mawili ya FC Barcelona yaliwekwa kimiani na wachezaji Lionel Messi na bao la pili likafungwa kwa ufundi wa hali ya juu na mchezaji Neymar. Hadi mwisho wa mchezo huo wa kundi F, PSG 3 na FC Barcelona 2.
Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy akifurahia jambo wakati alipofika katika uwanja wa Parc des Princes kushuhudia mchezo huo kati ya PSG na FC Barcelona hapo jana usiku.
MAPENZI MOTO MOTO!! Mwanamuziki mahiri wa Marekani, Jay Z akiwa na mkewe Beyonce katika uwanja wa Parc des Princes mjini Paris kushuhudia mchezo kati ya PSG na FC Barcelona jana usiku, mchezo uliomalizika kwa PSG kuibuka na ushindi wa mabao 3-2

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni