.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 23 Oktoba 2014

LIGI YA MABINGWA ULAYA, LIVERPOOL YATANDIKWA NYUMBANI 3-0 NA MABINGWA WATETEZI REAL MADRID

 Mabingwa watetezi wa kombe la ligi ya mabingwa Barani Ulaya, Real Madrid usiku wa kuamkia leo wameibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhid ya wenyeji wao Liverpool katika mchezo wa ligi ya mabingwa Barani Ulaya, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Anfiel.
Real Madrid ambayo ilisafiri toka Hispania, ilipata mabao yake kupitia kwa Cristiano Ronaldo ambaye alifunga bao lake katika dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza, kisha muuaji Karim Benzema akaongeza mabao mawili ya haraka haraka katika dakika za 30 na 40 kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza. 

Mabao hayo yalionekana kuwachanganya wenyeji Liverpool na kukubali kumalizika kwa dakika 90 wakiwa wametandikwa mabao 3-0.
 Tulia lazima nipite!! Isco akimpiga chenga ya maudhi Mario Balotelli wa Liverpool katika mchezo huo jana usiku.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni