Meli ya Uingereza imewasili Sierra
Leone kusaidia kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, katika
nchi za Afrika Magharibi.
Meli hiyo ya Royal Fleet Auxiliary
Argus imebeba shehena ya vyakula, vifaa tiba, pamoja na magari 32 ya
aina ya pick-up, katika kusaidia kukabiliana zaidi na virusi vya
Ebola.
Madaktari, wauguzi pamoja na
wanajeshi wa Uingereza wapo kwenye meli hiyo, iliyotia nanga katika
Jiji la Freetown.
Ugonjwa wa Ebola umeshauwa karibu
watu 5,000 waliopata maambukizi yake ambao zaidi ya watu 10,000
wakiwa katika nchi za Afrika ya Magharibi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni