.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 1 Oktoba 2014

MEYA WA BELL GARDENS, CALIFORNIA MAREKANI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MKEWE

                                                                     Meya Daniel Cerspo enzi za uhai wake. 

Meya wa Bell Gardens, California nchini Marekani, Daniel Crespo amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mkewe. 

Meya huyo mwenye miaka 45 amefariki dunia jana jumannne akiwa njiani kukimbizwa hospitali baada ya kupigwa risasi na mkewe Lyvette Crespo ( 43 ) katika kile kinachoelezewa kuwa ni baada ya kutokea majibizano baina yao wakiwa nyumbani kwao. 

Mkewe hivi sasa anashikiliwa na polisi. Wawili hao walifunga pingu za maisha mwaka 1986 na kufanikiwa kupata mtoto wa kiume, Daniel Jr ( 19 ) ambaye wakati wa tukio hilo la kuuawa kwa baba yake alijaribu kuwasuluhisha kabla ya mama yake kufyatua risasi na kumuua baba yake.
Polisi wakiwa wameshika doria nje ya nyumba ya Meya Daniel Crespo baada ya kupigwa risasi na mkewe.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni