Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akifurahia kazi za amali
zinazofanywa na akina Mama wa Vikundi vya Ushirika vya Jimbo la
Magomeni na kushawishika kununua mkeka wa asili ya Zanzibar.
Baadhi ya Wajumbe
wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania { UWT } Jimbo la Magomeni
wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi hayupo pichani akilifungua Baraza
hilo.
Mama Asha Suleiman Iddi akilifungua Baraza Kuu la UWT Jimbo la Magomeni kwe3nye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Tawi la Nyerere Mjini Zanzibar.
Picha zote na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Akinamama Nchini wana wajibu wa
kujiepusha na makundi ambayo ndio adui mkubwa katika harakati za
maendeleo na Kisiasa hasa wakati huu wa Taifa likikaribia kuelekea
katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi alisema hayo wakati akilifungua
Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania { UWT } Jimbo la Magomeni
linalofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Tawi la CCM Nyerere Wilaya ya
Mjini Zanzibar.
Mama Asha alisema njia pekee ya
kufikia maendeleo hayo ni kwa akina mama hao pamoja na wananchi wote
kufanya kazi zao kwa bidii na maarifa ili kufikia malengo
wanayojipangia kuyatekeleza.
Alisema kamwe hakutakuwa na miujiza itakayoletwa na baadhi ya watu kwa kutaka kufanikisha maslahi yao binafsi kupitia udanganyifu wanauelekeza kwa wananchi hasa wanawake ili kufikia azma yao.
Mama Asha alifahamisha kwamba CCM
ndio chama pekee Nchini Tanzania chenye uwezo wa kuwaletea maendeleo
wananchi kutokana na sera zake zenye uwezo wa kutekelezeka wakati
wote.
Aliwatahadharisha akina mama hao
kuwa na tahadhari na watu waliowahi kuneemeka na Serikali zilizopo
madarakani ambao wakati huu wamekuwa wakizipinga kwa vile wako nje ya
utumishi.
Alieleza kwamba ushawishi wa watu
hao ulifikia hatua ya kuwataka watu wawe vilema kwa sababu tu ya uchu
wao wa madaraka ya nchi hii bila ya kujali kuwa vitendo vyao hivyo
vina muekeo wa kujenga chuki za maisha ndani ya jamii.
Katika kuunga mkono vikundi vya
kiuchumi na ushirika vya akina mama hao wa Jimbo la Magomeni Mama
Asha alisema kupitia Umoja wao wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa
CCM Zanzibar wataangalia uwezekano wa kusaidia akina mama hao.
Aliuomba uongozi wa Umoja wa
Wanawake Tanzania { UWT } Jimbo la Magomeni kuviorodhesha vikundi
hivyo pamoja na muongozo wa shughuli wanazozifanya akina mama hao ili
vipatiwe msaada unastahiki kutokana na kazi zao.
Mapema akitoa taarifa fupi ya Umoja
wa Wanawake Tanzania Jimbo la Magomeni Katibu wa UWT Jimbo hilo Bibi
Maimuna Bara bara alisema akina mama wa Jimbo hilo wako imara
kuisubiri Katiba iliyopendekezwa na Bunge la Katiba kwa ajili ya
kuipigia kura ya ndio wakati ukiwadia.
Bibi Maimuna alisema akina Mama hao
wamewapongeza Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwa uwamuzi wao wa
kupendekeza Katiba inayotoa fursa sawa ya hamsini kwa hamsini
kijinsia kwenye nafasi za uongozi pamoja na maamuzi ya Taifa.
Alisema katika kukabiliana na ukali
wa kimaisha akina mama wa Jimbo hilo tayari wameshaanzisha vikundi 11
vya kuweka na kukopa sambamba pia na kuanzisha vikundi vya vikoba.
Hata hivyo Bibi Maimuna alieleza
kwamba zipo changa moto zilizojitokeza katika vikundi vyao akizitaja
kuwa ni pamoja na ufinyu wa elimu kwa wana vikundi, vitendea kazi
kama Kompyuta pamoja na ukosefu wa fedha za kuendeshea miradi yao.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
20/10/2014.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni