Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa
mfanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai iliyoko Beijing mara baada ya kuwasili
hotelini hapo. Mama Salma ameambatana na mumewe Rais Dkt. Jakaya Kikwete ambaye
amewasili nchini China tarehe 21.10.2014 kwa ziara ya kiserikali.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa Hoteli
ya Diaoyutai ya mjini Beijing mara baada ya kuwasili nchini China kwa ziara ya
kikazi tarehe 21.10.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Bwana Yang
Hua, Mmoja wa viongozi wakuu wa China National Offshore Oil Corporation
(CNOOC), wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa
Shirika hilo Bwana Wang Yilin kwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete alipotembelea makao
makuu ya Shirika hilo yaliyoko Beijing nchini China tarehe 22.10.2014. Shirika
hilo hujishughulisha na utafiti wa mafuta na gesi baharini, uchimbaji na uuzaji
wa maliasili hizo.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa China National
Offshore Oil Corporation Bwana Wang Yilin wakizindua rasmi mtambo mpya wa
utafutaji wa mafuta na gesi baharini, Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Makao
Makuu ya Shirika hilo huko Beijing tarehe 22.10.2014.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania
unaozuru nchini China wakiangalia vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na Shirika
la CNOOC la China katika kazi ya
utafutaji wa mafuta na gesi baharini wakati walipotembelea Makao Makuu ya
Shirika hilo huko Beijing tarehe 22.10.2014.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akishirikiana na Mkewe Mama Salma
Kikwete na Professa Li Songshan (kushoto kwa Rais Kikwete), Mwanzilishi wa
Kijiji cha Sanaa cha Afrika kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi
kijiji hicho kilichopo katika wilaya ya Songzhuang nchini China tarehe
22.10.2014.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia baadhi ya ngoma za asili
ya Afrika zilizokuwa zikipingwa na vijana wa kichina mara baada ya ufunguzi
rasmi wa kituo cha sanaa za Afrika huko Songzhuang tarehe 22.10.2014.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika
kitambaa maalum mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li
Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na
Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama.
Waanzilishi wa Kijiji cha Sanaa za Afrika Professa Li
Songshan na Mke wake Dkt. Han Rong wakimkabidhi zawadi ya picha Rais Dkt.
Jakaya Kikwete na Mke wake mara baada ya ufunguzi rasmi wa kijiji hicho tarehe
22.10.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiandika kumbukumbu yake
kwenye kijiji cha sanaa za Afrika mara baada ya Rais Dkt. Kikwete kuandika
kumbukumbu yake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni