.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 1 Oktoba 2014

MPAMBANO WA NGUMI KUPIGWA SIKU YA NYERERE DAY TANDIKA



BONDIA Imani Daudi anatarajia kupigana na Patrick Amote kutoka Kenya kwenye mpambano wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi utakaofanyika katika ukumbi wa Musoma Bar Tandika siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Nyerere Day tarehe 14 mwezi huu, mpambano huo unaoratibiwa na Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO chini ya Rais wake Yassin Abdallah 'Osthadhi' na lina malengo ya kumkumbuka Baba wa Taifa katika siku hiyo ya kipekee kabisa kwa nchi yetu ya Tanzania.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Abdallah amesema kuwa kila mwaka wanafanya hivyo kwa ajili ya kumkumbuka Baba wa Taifa hili ambaye alipenda michezo mbalimbali bila ubaguzi wa aina yoyote ile ingawa kwa sasa michezo inabaguliwa kwa mingine kupewa ufadhili na mingine kupewa kidogo na mingine kunyimwa kabisa ufadhili.

Aliongeza kuwa siku hiyo pia kutakuwa na mipambano mbalimbali ya utangulizi moja likiwa bondia Shomari Milundi atamenyana na Suma Ninja na mapambano mengine mbalimbali

Nae bondia Imani Daudi amejidhatiti kufanya kweli kwa kumsambalatisha Amote wa kenya ili aendeleze wimbi lake la ushindi na kuvutia mashabiki zaidi katika mchezo huo wa masumbwi.
Siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo. 

Pia kutakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni