.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 24 Oktoba 2014

MTOTO WA MWAKA MMOJA ATUMBUKIA KWENYE KISIMA CHA MAJI MACHAFU NA KUFA MBEYA

                                                 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                                                 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
                                                 JESHI LA POLISI TANZANIA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 24.10.2014.

MTOTO MDOGO WA MWAKA MMOJA NA NUSU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHA MAJI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA ITEZI AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO].

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KASUMULU BODA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTOTO MDOGO MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA NUSU [011/2] ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ELISHA JUMA MKAZI WA SHEWA ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHENYE MAJI MACHAFU.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 23.10.2014 MAJIRA YA SAA 07:00 ASUBUHI HUKO SHEWA, KATA YA MWAKIBETE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, KABLA YA TUKIO HILO, MAREHEMU ALIKUWA AKICHEZA MAENEO YA JIRANI NA KISIMA HICHO KILICHOKUWA NA MAJI MACHAFU YA MVUA YALIYOKUWA YAMEHIFADHIWA KWA AJILI YA SHUGHULI ZA UJENZI.

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA KITABIBU.


KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WADOGO IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA, ANATOA WITO KWA JAMII KUFUKIA MASHIMO, KUFUNIKA VISIMA NA MATUNDU YA MAJI MACHAFU KWANI NI HATARI KWA WATOTO WADOGO.

TAARIFA ZA MSAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AITWAYE MARIAM MASWALI (30) MKAZI WA ITEZI JIJINI MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 20.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 23.10.2014 MAJIRA YA SAA 13:30 MCHANA HUKO MAENEO YA ITEZI, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA NA POMBE HIYO NYUMBANI KWAKE. AIDHA, MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA MATENKI – BODA AITWAYE BARAKA WILLIAM (32) AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA BOSS KATONI 06 NA RIDDER KATONI 03.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 23.10.2014 MAJIRA YA SAA 16:10 JIONI HUKO MAENEO YA KASUMULU – BODA, KATA YA KASUMULU, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA NA POMBE HIZO ALIZOKUWA AMEZIBEBA KWENYE PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.638 BRU AINA YA SANLG.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE YA MOSHI PAMOJA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA, ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UINGIZAJI/USAMBAZAJI NA UUZAJI WA POMBE KALI NA POMBE YA MOSHI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

Imesainiwa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni