Mwanaume mmoja aliyepooza miguu
ameweza kutembea tena baada ya kufanyishwa mazoezi ya kitabibu pamoja
na kupandikizwa seli kwenye uti wake wa mgongo kwa kupitia kwenye
tundu za pua.
Tiba hiyo ambayo ni ya kwanza
kufanyika duniani, imefanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa
Poland kwa ushirikiano na wanasayansi wa London.
Mwanaume huyo Darek Fidyka, ambaye
alipooza sehemu ya mwili kuanzia kifuani hadi miguuni kufuatia
kushambuliwa na kisu mwaka 2010, hivi sasa anaweza kutembea kwa
msaada wa vifaa maalum.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni