Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu,
(Kulia), akiteta jambo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Afande Leonard
Paul, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa baadhi ya
wachezaji wa timu ya polisi mkoani Morogoro na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu wanaohudhuria
semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mkoani Morogoro, Alhamisi Oktoba
23, 2014.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu,
akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu ya Polisi Morogoro, Jumatano Oktoba
22, 2014, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa
wachezaji hao na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, wanaohudhuria semina
ya siku moja iliyuoandaliwa na Mfuko huo Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu,
akizungumza na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, wakati wa chakula cha
usiku kilichoandaliwa na Mfuko huo mjini Morogoro Oktoba 22, 2014. Wajumbe hao
wanatarajiwa kuhudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo ili
kuwaelimisha walimu faida wanazoweza kupata endapo watajiunga na Mfuko huo.
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni
wa PSPF, Mwanjaa Seme, akiwasalimia walimu ambao ni wajumbe kutoka idara ya
utumishi wa walimu wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa wajumbe hao
wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF, ili kuelezea shughuli
mbaklimbali na faida unazoweza kupata unapojiunga na Mfuko huo. Semina hiyo
ilifanyika mkoani Morogoro.
Msanii Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF, akiimba sambamba na baadhi ya walimu na maafisa wa Mfuko huo,
wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na PSPF, kwa wajumbe wa idara ya
utumishi wa walimu wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo
mkoani Morogoro. Picha na Masogange
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni