Rais wa Ghana John Mahama amesema
mahitaji muhimu pamoja na rasilimali za kubaliana na ugonjwa wa Ebola
zimeanza kuwasili katika nchi tatu za Afrika Magharibi zilizokumbwa
mno na ugonjwa huo.
Bw. Mahama ambaye ndie kiongozi wa
ushirikiano wa kikanda wa ECOWAS, ameviambia vyombo vya habari vituo
vya tiba vimeanzishwa katika nchi za Guinea, Liberia pamoja na
Sierra Leone.
Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola
umeshauwa watu 4,500 tangu kutokea mlipuko wake mapema mwaka huu,
huku vifo karibia vyote vikitokea katika nchi za Guinea, Liberia
pamoja na Sierra Leone.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni