Serikali ya Mali imethibitisha
kuwepo kwa mgonjwa wa kwanza wa Ebola katika nchi hiyo.
Mali imesema mgonjwa huyo mwenye
umri wa miaka miwili vipimo vimeonyesha anahoma ya virusi hivyo,
ambapo alirejea hivi karibuni akitokea Guinea.
Zaidi ya watu 4,800 wamekufa kwa
Ebola, idadi kubwa ikiwa katika nchi za Liberia, Guinea pamoja na
Sierra Leone tangu mwezi Machi.
Wakati huo huo timu ya wanasayansi
wa Kimataifa imekutana kujadili uwezekano wa kutumia damu ya wagonjwa
waliopona Ebola, kama tiba.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni