.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 21 Oktoba 2014

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI TABORA



Ndugu waandishi wa habari katika mkoa wetu wa Tabora kumetokea matukio yafuatayo:-

MAUAJI :- Huko kitongoji cha Mwamalutu kijiji/kata ya Nata wilaya ya Nzega na mkoa wa Tabora waliuawa watu watatu wafamilia moja ambao ni

1. RETICIA D/O THOMAS, 32yrs, msukuma mama mzazi wa watoto.

2. MARIETHA D/O NICOLOUS, 8yrs, msukuma

3. MAGRETH D/O NICOLAUS, 6yrs wote ni wanafunzi wa shule ya msingi mwamalulu waliuawa kwa kukatwa mapanga nyumbani kwao ambapo mwili wa marehemu RETETICIA ulikutwa sebuleni ukiwa umekatwa mapanga maeneo ya kichwani na mkono wa kulia wakati miili ya watoto ikiwa ipo chumbani kwao. 


Chanzo cha mauaji hayo inasadikiwa ni wivu wa mapenzi . Juhudi za kuwatafuta watuhumiwa waliohusika na mauaji hayo zinaendelea.  

MAUAJI :- Huko maeneo ya barabara ya Urambo eneo la kanisa katoliki la makokola Manspaa ya Tabora ulibainika mwili wa COSMAS S/O JOHN @BUTABUYE 40yrs Muha mkazi wa Ruwanzari dereva boda boda anayefanya shughuli zake katika eneo la four ways aliuawa kwa kuchomwa na kisu juu ya kiuno upande wa kulia na chini ya titi la kulia. 

Wauaji hao wamefanikiwa kupora pikipiki aina ya sunlg yenye namba za usajiri reg t.707 CYV rangi nyekundu. 

Aidha katika eneo la tukio kumekutwa kisu kimoja kinachodhaniwa ndicho kilichotumika kumchoma marehemu. 

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa kitete kwa uchunguzi zaidi. Juhudi za kuwatafuta watuhumiwa zinaendelea.

Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora linalaani kitendo hicho cha kiakatili, Pia tunazidi kutoa rai kwa wananchi kuacha matukio ya kihalifu kama hili. 


Aidha Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wengine na kutoa onyo kwa wale wote wanaofikiria kujihusisha na uhalifu kama huo na uhalifu wa aina nyingine yeyote.                                                                                        
                                                                                      Imetolewa na:- 
                                                                                Suzan Kaganda - ACP                                                                                                                                              
                                                            KAMANDA WA POLISI MKOA WA TABORA

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni