.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 20 Oktoba 2014

TFF, KLABU VPL WAJADILIANA KUBORESHA SOKA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) wamekutana mwishoni mwa wiki na kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha maendeleo ya mchezo huo nchini.

Mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam uliongozwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na kuhudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF pamoja na wanyeviti wa klabu za VPL.

Masuala yaliyozungumzwa ni leseni za klabu (club licensing), maboresho ya Taifa Stars, Kanuni za Ligi Kuu, Kombe la FA (Shirikisho) na mchango wa klabu hizo katika kuendeleza mpira wa miguu kwa vijana.

Uwasilishaji katika mkutano huo kuhusu maboresho ya Taifa Stars ulifanywa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Mart Nooij wakati leseni kwa klabu ulifanywa na Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura.

Kuhusu Kombe la FA, klabu zilifahamishwa kuwa mazungumzo kati ya TFF na mdhamini yanaendelea, ambapo zilikaribisha wazo hilo kwa vile michuano hiyo itatoa fursa kwa timu zao kucheza mechi nyingi za mashindano, hivyo kutoa nafasi ya kucheza kwa wachezaji wengi zaidi.

Bingwa wa michuano ya FA ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Rais Malinzi aliziomba klabu kukutana na kuwasilisha mapendekezo yao ya jinsi ya kuchangia/kuboresha maendeleo ya mpira wa miguu kwa vijana, kuboresha Kanuni za Ligi Kuu na kuboresha Kanuni za Bodi ya Ligi ili yaweze kufanyiwa kazi.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni