.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 31 Oktoba 2014

WAANDAMANAJI WAENDELEA KUSHINIKIZA RAIS BLAISE COMPARE AJIUZULU

Waandamaji makumi kwa maelfu wamekusanyika na kuandamana kwa siku ya pili nchini Burkina Faso kaika mji Mkuu wa Ouagadougou, wakimtaka rais Blaise Compaore kujiuzuru.

Viongozi wa upinzani jana usiku walitumia mitandao ya kijamii kuitisha maandamano mapya, wakionyesha kuchukizwa na rais Compaore ambaye alikaririwa baada ya maandamano ya siku ya kwanza kuwa ataendelea kuwa madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja akiongoza serikali ya mpito.

Katika tamko hilo rais Compaore pia alikubali kutogombea tena baada ya waandamanaji kuchoma majengo ya serikali.

Kuundwa kwa serikali ya mpito kulitangazwa na mkuu wa majeshi nchini humo Jenerali Honore Traore ambaye amesema atashirikisha vyama vyate vya siasa na pia alitangazwa kuvunjwa kwa bunge la nchi hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni