Ng'ombe watakuwa wanagaiwa kwa
wakinababa kaskazini mwa Kenya, ambao watahakikisha watoto wao wakike
wanaendelea na masomo.
Gavana wa kaunti ya Laikipia Joshua
Irungu, amesema ngombe tisa watagaiwa kwa wakinababa watakaotimiza
suala hilo katika maeneo yawafugaji vijijini.
Kwa mujibu wa sheria za Kenya, mzazi
atakayeshindwa kumpeleka mtoto wake shule anaweza kupatiwa adhabu ya
kifungo jela.
Hata hivyo ndoa za utotoni ni jambo
ambalo limezoeleka mno katika jamii za wafugaji, ambazo hutegemea
zaidi kupata mahari ya ng'ombe.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni