.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 28 Novemba 2014

COASTAL UNION U-20 KUCHEZA NA KOROGWE UNITED KESHO

TIMU ya Coastal Union U-20 ya Tanga Kesho Inatarajiwa kusafiri kuelekea wilayani Korogwe mkoani Tanga kucheza mechi ya kirafiki na Mabingwa wa soka wilaya ya Korogwe,Korogwe United mechi itakayochezwa uwanja wa Chuo cha Ualimu wilayani humo.

Akizungumza leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga,amesema kuwa maandalizi ya kuelekea mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa lengo likiwa kukipa makali kikosi hicho ambacho kinajiandaa na mashindano ya vijana hapa nchini.

Assenga amesema kikosi cha timu hiyo kitaondoka kesho(leo) saa sita mchana kwa kutumia usafiri wa basi la klabu hiyo wakiwa na viongozi mbalimbali wa klabu hiyo ambao watakwenda kushuhudia mchezo huo utakaokuwa wa kusisimua.

Amesema kuwa licha ya kucheza mechi hiyo lakini wataangalia uwezekano
wa kikosi hicho kucheza mechi nyengine za kirafiki ili kuweza kutimiza ndoto zao za kuhakikisha wanatetea vyema taji la ubingwa wa kombe la Uhai ambalo wanalishikilia.

Coastal Union U-20 tayari walishacheza mechi moja na timu ya Monga Stars wilayani Mkinga na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ambapo mkakati wa timu hiyo kucheza mechi nyengine za kirafiki utaendelea.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni