.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 21 Novemba 2014

COASTAL UNION UNDER 20 YAPANIA KUTETEA TAJI LA KOMBE LA UHAI

TIMU ya Coastal Union ya Vijana U-20 imepania kuhakikisha inatetea taji lake wanalolishikilia la Michuano ya Kombe la Uhai kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni hapa nchini.

Coastal Union U-20 ambao ni mabingwa wa kombe hilo mara baada ya kuifunga Yanga kwenye mechi ya Fainali ya Mashindano hayo msimu uliopita kwenye mchezo fainali ambao ulichezwa uwanja wa Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo,Meneja wa timu hiyo,Abdul Ubinde alisema kuwa maandalizi ya timu hiyo kuelekea michuano hiyo yanaendelea vizuri ambapo timu hiyo inaendelea na mazoezi yake kila siku kwenye uwanja wa soka Disuza asubuhi na jioni chini ya Kocha wake,Joseph Lazaro ambaye amepania kutetea taji hilo.

Ubinde amesema kuwa kwenye mashindano hayo msimu huu timu hiyo itaingia ikiwa na lengo moja la kuhakikisha wanapambana kufa na kupona ili kuweza kuendeleza kushikilia ubingwa wake kwa sababu ya uimara wa kikosi hicho.

Amesema kuwa hatuendi kushindana kwenye michuano hiyo bali kuhakikisha tunatetea taji letu la Ubingwa wa Michuano hiyo ambao sisi tunaingia kama mabingwa watetezi.
 

Ameongeza kuwa kikosi cha timu hiyo kimeimarika vilivyo na kipo tayari kushiriki mashindano hayo kwa mafanikio kutokana na kuwa na wachezaji mahiri wenye uwezo wa kuleta mapinduzi kwenye michuano hiyo.

Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji nguli akiwemo mlinda mlango namba mbili wa kikosi cha Coastal Union inayoshiriki ligi kuu Fikirini Suleiman “Mapara”Mohamed Twaha “Dijong”,Mtenje Albano na Mohamed Omari “Hungry”

Meneja huyo amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wapo kwenye morali wa kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kucheza kwa umakini mkubwa lengo likiwa kupata matokeo mazuri kila mechi watakayocheza.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni