Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika
mkutano huo wa hadhara, ambapo ameahidi kukutana wadau na viongozi wa mikoa ya
inayolima korosho nchini, ili wajadili kero mbalimbali za wakulima wa zao hilo
na kuzipatia ufumbuzi wa kudumu.
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, akielezea utekelezji wa
miradi mbalimbali jimboni humo wakati wa mkutano huo wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitembelea maghala
ya kuhifadhia korosho wilayani Tandahimba, Mtwara wakati wa ziara ya kuimarisha
uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi na
kupkea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Kinana akisaidia kumtwisha gunia la korosho mmoja wa
wapagazi wa maghala ya kuhifadhia korosho, wilayani Tandahimba leo.
WANANCHI wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia
katika Kata ya Mahuta, wilayani Tandahimba.
Aliyekuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Tandahimba, Jaffari
Hassan ambaye amehamia CCM, akielezea
sababu zilizosababisha ahamie chama hicho wakati wa mkutano wa hadhara, mjini
Tandahimba.Hassan hivi sasa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa wilaya hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni