.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 29 Novemba 2014

KHANGA PARTY NI LEO SAFARI CARNIVAL

                                                                                      Na Andrew Chale
USIKU maalum wa kuenzi vazi la Khanga na magwiji wa taarab nchini 'Usiku wa Khanga Party na Spice Modern Taarab' unapotarajia kulindima usiku wa leo Novemba 29 ndani ya Ukumbi wa Safari Carnival, Mikocheni B, karibu na daraja la Kawe, na kusindikizwa na gwiji wa mipasho Khadija Kopa pamoja na Bilal Mashauzi.

Kwa mujibu wa Mama wa Mitindo Bi. Asia Idarous Khamsin amebainisha kuwa kwa ushirikiano wa Fabak Fashions na Safari Carnival wameandaa usiku huo maalum kuenzi vazi la Khanga.

"Usiku wa Khanga Party na Spice Modern Taarab ni maalum kuenzi vazi hili la khanga ambapo pia watu wote watakaofika watavaa vazi maalum la khanga. Hivyo wadau wajitokeze kwa wingi kwa kiingilio cha sh 10,000 na 20,000 kwa V.I.P." alisema Asia Idarous Khamisin.

Aidha, alisema wadau watafurahia muziki mzuri kutoka kwa magwiji wa taarab hapa nchini akiwemo Khadija Kopa, Spice Modern taaba na Bilal Mashauzi.

Amesema leo usiku pia kutakuwa na zulia jekundu (Red Carpet) ambapo watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa na watu maarufu watakaojitokeza, ambao pia The Legend Dj John Dilinga wa nIsumba Lounge atasimamia muziki Old School.

Pia alibainisha kuwa, tayari tiketi zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwemo Fabak fashions Mikocheni na Safari Carnival.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni