.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 20 Novemba 2014

KUFUZU KWA IVORY COAST - AFCON 2015 KWAZUA BALAA, MASHABIKI WAPAMBANA NA POLISI BAADA YA MCHEZO DHIDI YA CAMEROON

Polisi wa Ivory Coast akimtandika virungu mmoja wa mashabiki ambaye yeye na wenzake waliuvamia uwanja baada ya timu yao ya taifa kutoka sare ya kutofungana na Cameroon na kufanikiwa kupata tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika mwakani huko Equatorial Guinea.
 Polisi akitembeza bakora kwa mashabiki waliovamia uwanja baada ya mpira kumalizika
Mashabiki wa Ivory Coast wakiwa wamening'inia katika goli hadi likapinda kuonyesha furaha yao baada ya timu yao kufuzu kwa Afcon mwakani huko Equatorial Guinea.
 Weweee muachie!! Askari polisi akijaribu kumtoa shabiki huyu ambaye alimkumbatia kwa furaha mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Gervinho baada ya mchezo wao dhidi ya Cameroon kumalizika.
Mamia ya mashabiki wa timu ya taifa ya Ivory Coast wakiwa wamejazana ndani ya uwanja baada ya mchezo baina ya timu yao na Cameroon kumalizika kwa sare ya kutofungana. Matokeo hayo yameivusha Ivory Coast kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwakani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni