Mahakama ya rufaa ya nchini Sweden
imekazia hukumu ya hati ya kukamatwa muasisi wa Wikileaks, Julian
Assange, na kuhojiwa kwa kesi ya udhalilishaji wa kingono.
Mahakama hiyo ya rufaa imekataa ombi
la rufaa ya Assange, ya kutengua amri ya kukamatwa kwake iliyotolewa
mnamo mwaka 2010.
Assange, ambaye amekanusha tuhuma
hizo amepatiwa hifadhi katika ubalozi wa Ecuador Jijini London nchini
Uingereza.
Mbali na kuhitajika Sweden kwa kesi
hiyo, Assange anahitajika nchini Marekani kwa kosa la kuvujisha siri
za nchi hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni