.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 21 Novemba 2014

POLISI WATANDA MOMBASA HII LEO KUZUIA WAUMINI KUINGIA KATIKA MISIKITI ILIYOFUNGWA

Ulinzi mkali wa polisi umewekwa leo katika eneo la Mwandoni la Kisauni, Kaunti ya Mombasa nchini Kenya kabla ya swala ya Ijumaa.

Hatua hiyo inafutia kufungwa kwa misikiti ya Swafaa na Minaa ambayo polisi wamedai inatumika kuwatumbukiza vijana katika itikadi kali za kidini.

Polisi wamesema jana usiku, vijana walijaribu kuingia kwenye msikiti Swafaa kwa ajili ya swala ya saa mbili usiku, lakini walidhibitiwa na maafisa usalama.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni