Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe
amevunja bunge, ili kutoa fursa ya kufanyika uchaguzi wa dharura,
utakaofanyika kati kati ya mwezi Desemba, mwaka huu.
Bw. Abe anajaribu kupata ridhaa mpya
ya kufanya mabadiliko ya kiuchumi, na anachelewesha suala
lisilokubalika la kuongeza kodi ya mauzo.
Hata hivyo kura ya maoni iliyofanywa
na vyombo vya habari vya Japan, inaonyesha idadi ndogo wanamuunga
mkono Bw. Abe, huku wengi wao hawamuelewi kwanini kaitisha uchaguzi
wa dharura ikiwa imebakia miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni