.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 22 Desemba 2014

DEREVA ALIYEKUWA AKITAMKA MUNGU MKUBWA AWAGONGA WATU 11 UFARANSA

Dereva aliyekuwa akitamka kwa kiarabu maneno yanayomaanisha 'Mungu ni Mkubwa', amewagonga watembea kwa miguu katika eneo la Dijon nchini Ufaransa na kuwajeruhi watu 11, wawili kati yao wapo mahututi.

Mtu huyo alikamatwa baada ya kuwalenga kuwagonga watu katika maeneo matano tofauti ya mji huo, katika muda usiozidi tafuati ya nusu saa.

Inasemekana mtu huyo akili zake hazikuwa zimetulia, na alikuwa akitibiwa kwenye hospitali za wagonjwa wa akili.

Polisi wa Ufaransa siku ya jumamosi walimpiga risasi na kufa mwanaume mmoja aliyekuwa akitaka kuwashambulia kwa kisu huku akitamka kwa sauti 'Mungu ni Mkubwa'.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni