Nchi ya Liberia imechelewesha mpango
wake ya kufungua shule, kutokana na madai kuwa haijajiandaa
kikamilifu kuzuia kusambaa kwa ugonjwa hatari wa Ebola.
Shule zilifungwa tangu Julai mwaka
jana, zilipaswa kufunguliwa siku ya jumatatu, hata hivyo sasa masomo
yataanza ifikapo Februari 16.
Shule kadhaa Liberia bado
hazijajiandaa kudhibiti Ebola, nyingi zikiwa hazina maji yenye
klorini kwa ajili ya wanafunzi kuosha mikono yao, pamoja na kipima
joto cha kubaini iwapo mwanafunzi anahoma.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni